Kuadhimisha Siku ya Kukosha Mikono
15 Oktoba 2008Matangazo
Hapa Ujerumani leo inaadhimishwa siku ya kukosha mikono. Kwa baadhi yetu tunaona kukosha mikono kabla ya kula au baada ya ktoka msalani ni jambo la kawaida, lakini lina umuhimu, si tu katika kuweka unadhifu wa mwili, lakini pia afya yako. Tunajikinga na magonjwa mengi sana, ikiwa tunaiendeleza desturi hiyo, na hilo si suala la uzungu au Uafrika, lakini ni jambo muhimu kwetu sisi sote. Nimempigia simu alasiri hii Daktari wa Kiswahili aliyeishi kwa karibu miaka 40 hapa Ujerumani atuelezee faida za mila hiyo ya kukosha mikono. Anazungumza na Deutsche Welle.